Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Jumatatu Januari 3, 2022 imepanga kutoa uamuzi mdogo wa pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.

Desemba 29 mwaka jana, mahakama hiyo ilishindwa kutoa uamuzi huo baada ya mawakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani.

Hata hivyo Desemba 17 mwaka jana, akiwasilisha hoja ya pingamizi hilo Wakili Mosses Mahuna aliieleza kuwa shahidi huyo hana uwezo wa kutambua watu kupitia ripoti ambayo hajaiandaa na wala si mtaalamu kutoka maabara ya kiuchunguzi.

Mawakili wa Serikali waliomba mahakama kutupilia mbali pingamizi hilo, kwani halina misingi ya kisheria wala mashiko.

Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapotoa uamuzi huo.

Ndugai amuomba radhi Rais Samia
Vyombo vya usalama barabarani vyatakiwa kuwa makini