Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa Gati ya Mkokotoni, unalenga kuimarisha utoaji wa huduma ili ziweze kuwa bora na endelevu, sambamba na kuufungua kiuchumi Mkoa Kaskazini Unguja.
 
Dk. Mwinyi amesema hayo  katika hafla ya  Ufunguzi wa Gati ya Mkokotoni, Mkoa Kaskazini Unguja, ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema ujenzi wa Gati ya Mkokotoni una dhamira ya kuimarisha utoaji wa huduma ili ziweze kuwa bora na endelevu kwa abiria wanaotumia Bandari hiyo pamoja na mizigo mchanganyiko


 
Alisema mradi huo unalenga  kuufungua Mkoa huo kiuchumi, wakati ambapo malengo ya Serikali ni kuiboresha zaidi Bandari hiyo ili kuziwezesha meli kubwa kutumia Bandari hiyo,

Eric Omondi atangaza kuvamia faragha za wasanii wa Kenya
Rais Samia amuwashia moto ‘Ndugai’, asema ana stress za 2025