Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema klabu hiyo itaendelea kumpa nafasi Abdihamid Moalin ‘Master Lecturer’ kama Kaimu Kocha Mkuu katika kipindi hiki cha Msimu wa 2021/22.

Abdihamid alikabidhiwa jukumu la kusimamia Benchi la Ufundi la Azam FC, baada ya kuondoka kwa Kocha George Lwandamina ‘CHIKEN’ kufuatia mambo kumuendea mrama.

Popat ametoa kauli hiyo huku Azam FC ikiwezeshwa na Kocha huyo kutoka nchini Marekani mwenye asili ya Somalia kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Amesema Uongozi wa Azam FC unaamini kwa Abdulhamid, hivyo hauna haraka wa kuanza mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu katika kipindi hiki ambacho kikosi chao kimeonesha kutulia na kupata matokeo.

“Niseme tu mpaka sasa hivi tumeamua kuendelea naye huyu kocha mpaka tutakapomaliza Mapinduzi. Tukimaliza hapo tutafanya tathmini” amesema Popat

Abdulhamid aliajiriwa klabuni hapo kama Mkurugenzi wa Ufundi mwishoni mwa mwaka 2021, na tangu alipokabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi cha Azam FC amekua na matokeo mazuri, huku akipoteza mchezo mmoja dhidi ya Simba SC kwa kufungwa mabao 2-1.

Dkt. Tulia achukua nafasi ya USpika wa Bunge
Barbara awatuliza Mashabiki, Wanachama Simba SC