Mwanaume wa Marekani David Bennett mwenye umri wa miaka 57 amekuwa mtu wa kwanza duniani kuwekewa moyo wa nguruwe aliyebadilishwa vinasaba(GMO).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madaftari Bennett, anaendelea vyema siku tatu baada ya upasuaji wa majaribio hayo uliofanyika katika mji wa Baltimore.
Aidha Upandikizaji wa moyo huo unachukuliwa kama matumaini ya kuyaokoa maisha a Bw Bennett, ingawa haijawa wazi bado ni fursa ya kiasi gani aliyo nayo ya kuishi maisha marefu
Madaktari wa Chuo Kikuu cha Maryland kituo cha tiba walipewa idhini maalum na wasimamizi wa matibabu kuendelea na upasuaji huo, kwa misingi kwamba vinginevyo Bennet angekufa,
Bennett alionekana uwezo wa kupandikiziwa moyo wa binadamu, uamuazi ambao mara nyingi huchukuliwa na madaktari wakati mgonjwa anapokuwa na afya duni.
Hatahivyo Bennett, anamatumaini kuwa upandikizaji wake wa moyo wa nguruwe utamuwezesha kuendelea na maisha yake.
Uwezekano wa kutumia viungo vya Wanyama kwa ajili ya kile kinachoitwa xenotransplantation ili kufikia mahitaji umekuwa ukifikiriwa kwa muda mrefu, na matumizi ya mishipa ya moyo wa nguruwe tayari limekuwa ni jambo la kawaida.
Mwezi Oktoba, 2021, madaktari wa upasuaji mjini New York walitangaza kwamba wamefanikiwa kupandikiza figo la nguruwe kwa binadamu.