Licha ya kutokuwepo kwenye kikosi cha Simba SC kitakachoikabili Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu leo Jumatatu (Januari 17), kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama ameuteka Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Chama amerejea Msimbazi kupitia Dirisha Dogo la Usajili, baada ya kuvunja mkataba na klabu ya RS Berkane ya Morocco iliyomsajili mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba SC.
Kiungo huyo amepokewa shangwe kubwa kutoka kwa Mashabiki wa Simba SC waliofika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu.
Chama alipanda gari moja na wachezaji wa Simba SC huku akiwa amevaa sare za kawaida za klabu hiyo, na viongozi walimuongoza, wakati wenzake wakishuka kwenye gari.
Chama alibaki kwenye gari hadi wachezaji wote wa Simba waliposhuka, na ndipo yeye pekee yake alitoka nje na kuwashangilia Mashabiki waliokua wanamsubiri kwa hamu kubwa.