Hatimaye mwanamuzuki Chris Brown ameibuka na kujibu tuhuma za kesi ya ubakaji inayomkabili baada ya mwanamke mmoja kumshtaki na kudai fidia ya dola milioni 20 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni 46 za Kitanzania.

Taarifa za awali zinasema mwanamke aitwaye Jane Doe alidai kufanyiwa kitendo cha ubakaji kwenye boti nyumbani kwa Diddy Miami Star Irland, alipokwenda kwa madai ya kuitikia wito wa Chris brown ambaye alisema kuwa ni rafiki wa kawaida na si mpenzi wake.

Kufuatia shutuma hizo, Chris Brown ameweka wazi kuwa tuhuma hizo ni mpango wa siri wenye kusukwa kwa lengo la kumdhoofisha kimuziki kwa kuwa si mara ya kwanza kwa yeye kufanyiwa visa vya kutengenezwa vyenye mfumo wa namna hiyo ili kumvurugia kazi zake.

“Natumai nyote mnaliona hili, wakati wowote ninapotoa muziki mpya au mradi, wanajaribu kuleta vitu vyao vya kipuuzi” aliandika Chris kupitia ukurasa wake wa mtamdao wa Instagram (Insta story).

Licha ya hilo nyota huyo hajadokeza chochote kuhusu mwenendo wa kesi hiyo kwa upande wake na hata namna anavyopambana kukabiliana na shutuma hizo nzito.

Chris Browm kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘IFFY’ aliouachia takriban wiki mbili zilizopita huku ukiwa umefanikiwa kupata watazamaji zaidi ya milioni 9 kwenye mtandao wa Youtube.

Waziri Jafo ateta na wanaunguja
Rapa Big Sean athibitisha kuwa na asili ya Nigeria