Juma Haji Duni ameshinda na kuwa mwenyekiti wa chama Cha ACT WAZALENDO baada ya kumshinda mpinzani wake Hamad Masud Hamad .

Katika uchaguzi ulifanyika January 29 Juma Haji Duni akipata kura 339 dhidi ya 125 za mpinzani wake.

Juma Haji Duni amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho anakuwa mwenyekiti wa tatu tangu kuasisiwa kwa chama hicho mwaka 2014.

Mwenyekiti wa kwanza ni hayati Anna Mghwira wa pili ni hayati Maalim Seif Sharif Hamad na sasa ni Juma Haji Duni.

Juma Haji Duni alikuwa mgombea mwenza wa mgombea wa chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ambae ni waziri mkuu wa zamani wa Tanzania mheshimiwa Edward Lowasa katika uchaguzi wa mwaka 2015.

ACT NA HOSTORIA….
Wenyeviti wote wa chama Cha ACT wamewahi kuwania nafasi za Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Hayati Anna Mghwira mwenyekiti wa kwanza wa ACT aligombea Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2015.

Hayati Maalim Seif Sharif Hamad aligombea Urais wa Zanzibar kwa nyakati tofauti na Juma Haji Duni alikuwa mgombea mwenza wa mgombea Urais wa CHADEMA mwaka 2015 kulingana na makubaliano kati ya CHADEMA NA CUF kuhusu wagombea mwaka 2015.

ACT pia inaingia katika historia nyingine tangu marekebisho ya katiba ya Zanzibar imetoa makamu wa kwanza wa Rais mara mbili.

Waziri wa TAMISEMI ametoa maagizo kwa Halmashauri zote nchi
Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi