Shahidi wa 12 katika kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, leo ataendelea kuhojiwa ikiwa na mawakili wa utetezi kuhusiana na ushahidi alioutoa.

 Shahidi huyo, Luteni Denis Urio wa upande wa mashtaka ataendelea kuhojiwa na kiongozi wa jopo la utetezi, Peter Kibatala katika hatua ya udodosaji.

Mchuano baina ya Luteni Urio na mawakili wa utetezi ulianza Alhamisi, baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake wa msingi aliouanza Jumatano ya wiki iliyopita huku akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Luteni Urio katika ushahidi wake alieleza alionana na Mbowe kwa mara ya kwanza mwaka 2012, jijni Dar es Salaam.

Alieleza kuwa Mbowe alitaka kujua msimamo wake kwa vyama vya upinzani, lakini yeye akamjibu kuwa kwa taratibu za kazi yake haruhusiwi kufungamana na chama chochote isipokuwa kwa kiongozi anayekuwa madarakani kwa wakati huo.

Alisema kuwa ingawa alimkubalia, hakuweza kuvumilia kukaa na taarifa hizo, hivyo alimtaarifu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz wakati huo, ambaye alimtaka aendelee kumpa Mbowe ushirikiano huku akiendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Pia aliieleza kwamba katika mchakato huo alipokea jumla ya Sh699,000 kutoka kwa Mbowe kwa ajili ya kuwawezesha vijana aliokuwa amemtafutia Mbowe na kwamba baada ya kumtafutia vijana hao, Mbowe alikata mawasiliano.

Itakumbukwa, Ijumaa iliyopita, Kibatala pekee alitumia zaidi ya saa tatu kumhoji na badaalilieleza Mwananchi kuwa bado ana maswali yatakayoweza kuchukua saa tatu leo

Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi juu ya askari aliyejinyonga
Harakati za uchaguzi Kenya:Ruto amtaka Kenyatta kukumbuka fadhila