Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar umekanusha taarifa zinazoendelea kusambaa mitandaoni zikidai kuwa, mchezo wao dhidi ya Young Africans umehamishiwa Mkoani Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu hiyo ya Mkoani Morogoro, imeleeza kuwa, hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa kuhusu mchezo huo kuhamishiwa mkoani Tabora.

Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo imeeza: “MANUNGU COMPLEX (Machinjioni) ndio uwanja wetu wa nyumbani na ndipo tutakapocheza michezo yetu YOTE ya nyumbani kwa michuano yote.”

“Taarifa inayosambaa kuwa tumechagua kiwanja tofauti na Manungu IPUUZWE…!”
“Karibuni TURIANI.”

Tayari Mtibwa Sugar imeshacheza dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Manungu Complex mwezi huu, baada ya Bodi ya Ligi Kuufunguliwa Uwanja huo.


Mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Young Africans umepangwa kuchezwa Februari 23, Uwanja wa Manungu Complex.

ASFC: Simba, Young Africans zabaki Dar es salaam
Channel za bure zarudishwa DSTV