Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ Simba SC watakutana Ruvu Shooting katika hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo msimu huu 2021/22.

Simba SC imevuka hatua ya 32 Bora kwa kuichapa Dar City FC mabao 6-0, jana Jumapili (Januari 30) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Ruvu Shooting wao waliiondosha KMC FC katika hatua ya 32 kwa changamoto ya Mikwaju ya Penati, juzi Jumamosi (Januari 29) Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Timu hizo zilifikia hatua ya kupigiana mikwaju ya Penati, baada ya matokeo ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Young Africans ambao walifika hatua ya Fainali msimu uliopita na kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Simba SC mjini Kigoma, nayo imetinga hatua ya 16 na itacheza dhidi ya Biashara United Mara.

Young Africans ilivuka hatua ya 32 Bora, kwa kuichapa Mbao FC juzi Jumamosi (Januari 29), katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, huku Biashara United Mara wakiibanjua Mbaya Kwanza FC mabao 2-1.

Michezo mingine ya hatau ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’


•Pamba v Dodoma Jiji
•Tanzania Prisons v Polisi Tanzania
•Coastal Union v Mtibwa Sugar
•Kagera Sugar v Namungo
•Baga Friends v Azam FC
•Mbuni/Lipuli v Geita Gold

Greenwood mikononi mwa Polisi
Mtibwa Sugar kuikabili Young Africans Manungu