.Serikali imetumia zaidi ya Billioni tisa kufanya matengenezo ya meli ya Mv Mbeya II iliyopata hitilafu iliyotokea wakati wa dhoruba mwezi Machi mwaka 2021 ilipokuwa ikitia nanga katika bandari ya Matema.

Akizindua safari za meli meli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, leo januari 31, 2022 amesema kukamilika kwa matengenezo ya meli hiyo imekuwa ni ukombozi kwa wakazi wa Wilaya na Mkoa kwani waliokosa huduma hiyo kwa muda mrefu.

Akizungumza Katika uzinduzi wa meli hiyo ambayo tayari imepewa cheti na taasisi ya udhibiti wa vyombo vya maji TASAC,Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari ya Itunge Abdalah Mohamed, amesema tayari matengenezo yamekamilika kwa asilimia mia moja na utoaji huduma utaendelea.

Meli ya Mv Mbeya II leo imeanza kufanya safari zake mkoa wa Ruvuma na Njombe baada ya kupata hitilafu miezi tisa iliyopita ikiwa na abiria zaidi ya mia moja na hamsini.

Amewataka wafanyakazi wa meli hiyo kuwa waaminifu na wazalendo katika kutoa taarifa pale wanapobaini kuna uharibifu ndani ya meli hiyo.

Baadhi ya abilia walioanza safari wameishukuru serikali kwa kufanya ukarabati huo na kupata ahueni ya usafirishaji wa bidhaa zao ambapo awali ulitumia alikuwa wakitembe a umbali mrefu

Rais awaapisha viongozi aliowateua
Pongezi za Young Africans zamuibua Ahmed Ally