Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha watendaji mbali mbali aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa zao.

Hafla hiyo ya kiapo imefanyika Ikulu Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi wakuu wa Kitaifa, Mawaziri, Viongozi wa Vyama vya siasa, Viongozi wa Dini pamoja na Wanafamilia.

Viongozi walioapishwa kushika nyadhifa hizo ni pamoja na Jaji Aziza Idd Sued alieteliwa kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Rufaa ya Idara Maalum za SMZ pamoja na Dk. Said Seif Mzee alieteuliwa kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Mwengine ni Dkt. Rahma Salim Mahafoudh alieteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Mbeya City yatuma salamu Young Africans
Ujio mpya wa meli ya MV Mbeya II