Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Kibu Denis, ataukosa mchezo wa Mzunguuko wa 14 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons, utakaounguruma kesho Alhamis (Februari 03) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kibu Denis alipata majeraha ya mguu akiwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City FC, ambapo Simba SC ilipoteza kwa kufungwa 1-0, Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya majuma matatu yaliyopita.

Kocha Msaidizi wa Simba SC Selemeni Matola amethibitisha kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jumatano (Februari 02) mchana jijini Dar es salaam, ambapo amesema Mshambuliaji huyo bado anaendelea na matibabu.

“Kibu Denis ataendelea kuwa nje ya kikosi kutokana na jeraha lake la mguu, tulitamani tuwe naye lakini kwa hali yake ni ngumu hadi atakapopona kabisa.” Amesema Matola

Kibu Denis tayari ameshaifungia Simba SC mabao matatu katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ukiwa msimu wake wa kwanza kuwatumikia mabingwa hao mara nne mfululizo akitokea Mbeya City.

Nizar Khalfan: Tunaiheshimu Ruvu Shooting
Simba SC yaahidi ushindi dhidi ya TZ Prisons