Tanzania imetajwa kufanya vizuri katika Sekta Ndogo ya Uchimbaji Mdogo wa Madini kutokana na usimamizi madhubuti uliopelekea ukuaji wa shughuli za uchimbaji mdogo hatua ambayo imeifanya nchi ya Zimbabwe kupanga kuwaleta wataalam wake kujifunza zaidi katika eneo hilo.

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko ameyasema hayo wakati akizungumza na Vyombo vya Habari mara baada ya kikao chake na Waziri wa Madini wa Zimbabwe Wiston Chitando, wataalam kutoka nchi hizo pamoja na Sekretarieti ya Umoja wa Nchi zinazozalisha Madini ya Almasi (Association of Diamond Producing Countries – ADPA) na Kimberly Processing Certification System (KPCS) ambayo imeshiriki kwa njia ya mtandao.

Dkt. Biteko amesema nchi hizo zimekutana kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa sekta ya madini pamoja na kujifunza namna bora ya kushirikiana kimaendeleo kwa nchi wazalishaji wa madini ya Almasi Barani Afrika.

Waziri wa Madini Dkt.Doto Biteko akizungumza na Waziri wa Madini Zimbabwe Wiston Chitanda.

Pia, ameongeza kuwa, kikao hicho kimelenga kuiwezesha nchi ya Zimbabwe kama mwenyekiti mtarajiwa wa umoja huo kujifunza namna ya kusimamia masuala yanayohusu umoja huo pamoja na kupata mrejesho wa namna shughuli zake zinavyoendelea kabla nchi hiyo haijachukua kijiti cha uenyekiti.

Aidha, Waziri Biteko amesema Tanzania inayo mengi iliyojifunza kutoka nchi ya Zimbabwe ambayo ni miongoni mwa nchi zilizoanza shughuli za uchimbaji madini kwa muda mrefu ambapo hivi sasa Sekta ya Madini katika nchi hiyo inachangia asilimia 12 katika Pato lake la Taifa ikilinganishwa na Tanzania ambayo hivi sasa mchango wake umefikia asilimia 9.7.

Ameongeza kuwa, pamoja na mafanikio hayo, bado nchi hiyo inakabiliwa na changamoto ya utoroshwaji wa madini hivyo uwepo wake nchini utaiwezesha kujifunza masuala ya udhibiti wa utoroshwaji madini ikiwemo kuwa na Sheria nzuri itakayosaidia kuwepo mabadiliko ya kisekta kama ilivyo kwa Tanzania.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Zimbabwe Wiston Chitando amesema kuwa haina shaka kuwa Tanzania imekuwa mfano mzuri kwa nchi hiyo kutokana na inavyosimamia Sekta ya madini hususan uchimbaji mdogo wa madini hali ambayo inailazimu nchi hiyo kuwatuma tena watalaam wake kuja nchini kujifunza zaidi ili kui

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 3, 2022
Ahmed Ally: Wameongeza MAKELELE sio ubora wa KIKOSI