Rais wa Jamhuri ya Muunganonwa Tanzania Samia Suluhu Hassn ametengua uteuzi wa Wakurugenzi 4 wa Halmashauri kwa matumizi mabaya ya Fedha za miradi ya maendeleo hususan ni zile za Ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Wakurugenzi hao ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza, Manispaa ya Singida – Mkoani Singida, Halmashauri ya Jiji la Mbeya – Mkoani Mbeya na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.

Akizungumza mbele ya Rais Samia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Innocent Bashungwa amesema halmashauri zote ambazo zimetuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi uchunguzi umefanyika na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita uchunguzi unaendelea.

Aidha Rais Samia ameagiza uchunguzi uendelee katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo napo kuna tuhuma za namna hiyo.

Manara, Ahmed Ally wabamizana mtandaoni
Ismail Rage apaza sauti kusua kwa Simba SC