Wamiliki wa mtandao wa Facebook kwa sasa, wanapitia wakati mgumu kibiashara, punde baada kupoteza kiasi cha pesa kisichopungua Usd 237 Billion ambazo ni sawa na zaidi ya Trilioni 547.9 za Kitanzania.

Kiwango hicho ni cha pesa ya hisa za kampuni hiyo ndani ya siku moja, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuingia hasara yenye ukubwa wa kiasi hicho tangu kampuni hiyo ianze kufanya kazi.

Hasara hiyo kwa kampuni ya Facebook ambayo miezi michache iliyopita ilibadilisha jina na kuwa Meta, imesababisha kuathiri sehemu ya utajiri wa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg ambaye amepoteza Usd 29.7 million, ambazo ni sawa na zaidi ya Trilioni 67 za Kitanzania.

Kwa mujibu wa chati ya orodha ya watu matajiri zaidi Duniani, Jumatano Februari 2, 2022. Mark Zuckerberg alishika nafasi ya 7 kwenye orodha ya watu matajiri zaidi duniani akimiliki kiasi cha pesa kisichopungua Usd 113 billion, ambazo ni sawa na zaidi ya Trilioni 261 za Kitanzania.

Baada ya tukio hilo, mpaka kufika siku ya Alhamis Februari 3, 2022 Mack ameshuka mpaka kwenye nafasi ya 12, huku kiwango cha utajiri wake kikiwa ni Usd 83.4 billion ambazo ni sawa na zaidi ya TSh. Trilioni 192 za Kitanzania.

Licha ya hilo, ripoti zinasema kuwa mtandao wa Facebook pia umeshuka kwa kiwango kikubwa kwa upande wa watumiaji wa mtandao huo maarufu Duniani kutokana na kipimo cha idadi ya watumiaji wa siku ‘Daily Active Users’.

Wakati huo ukipoteza watumiaji takribani laki tano (500k) ndani ya kipindi cha takriban miaka 18 ya utendaji wa mtandao huo, idadi ya watumiaji  ikiporomoka kutoka watumiaji Bilioni 1.93 hadi kufikia watumiaji Bilioni 1.92.

Waliosababisha kifo cha Michael K. Williams wanaswa
Manara, Ahmed Ally wabamizana mtandaoni