Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Chongolo ameongoza viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi katika Matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi yanayofanyika kitaifa Mkoani Mara, Leo Februali 05, 2022.
Matembezi hayo yameanzia maeno ya ikulu ndogo ya mjini Musoma na kupita katika mitaa ya mji wa Musoma na kuhitimishwa katika ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara.
Matembezi hayo yatafuatiwa na Sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi yatakayifanyika uwanja wa Karume ambapo mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.