Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuhakikisha Mameneja TARURA wa Mkoa yote nchini wanatoa Ripoti kila mwezi kuhusu kazi zao kwa kuwa moja ya kigezo cha kuwapima ni utendaji kazi uliotukuka.

Bashungwa ametoa agizo hilo Leo Februari 6, 2022 wakati wa uwekaji wa Jiwe la msingi kwenye Mradi wa Majisafi wa Mugambo-Kiabakari-Butiama katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.

Amesema kazi ya Mameneja Mkoa ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara zinasimamiwa kwa weledi na kuhakikisha thamani ya fedha ya fedha inaonekana kwenye ubora wa miundombinu ya barabara inayotekelezwa.

Amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI inaendelea kufanya maboresho kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili iweze kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa na Serikali katika ujenzi ya miundombinu ya barabara nchini ili kuwafungulia wananchi barabara za vijijini na kufika kusikofikika.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 7, 2022
Watoto wafariki kwa kukosa hewa