Viongozi wa Afrika wamelalamikia “wimbi” la mapinduzi, baada ya kutokea mapinduzi ya kijeshi mara tano katika mwaka uliopita na tayari mara moja mapmea mwaka huu.

Wakati fulani idadi ya mapinduzi barani Afrika ilipungua, baada ya kuenea kwa chaguzi na uhamishaji wa madaraka kwa njia ya amani.

Nchi mbili ambazo jeshi limenyakua mamlaka hivi karibuni ambazo ni Burkina Faso na Mali zimekuwa zikijitahidi kuzuia uasi wa Kiislamu.

Wiki iliyopita, kulikuwa na jaribio la mapinduzi nchini Guinea-Bissau, ambalo rais alilaumu magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Nchi hiyo iko kwenye sehemu kuu ya usafiri kati ya nchi zinazozalisha kokeini katika Amerika ya Kusini na masoko ya Ulaya.

Wiki iliyopita, Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo alisema mapinduzi nchini Mali yamekuwa “ya kuambukiza”, na kuwafanya maafisa wa kijeshi katika majirani zake wa Afrika Magharibi, Guinea na Burkina Faso, kuiga mfano huo.

Wakati mapinduzi ya Afrika Magharibi yakikaribishwa na watu wengi katika nchi hizo, hatua ya jeshi kuchukua madaraka nchini Sudan mnamo Oktoba 2021 imesababisha maandamano makubwa mitaani ya kudai kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.

Haya yamekabiliwa na nguvu zisizo na huruma, ambapo makumi ya waandamanaji wameuawa na waathirika wakuu wamekuwa ni watoto na wanawake.

Jack Wilshere akata tamaa Arsenal
Viongozi wa Serikali Mara mashakani kutumbuliwa