KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati kufanya kazi kwa uadilifu, ubunifu na weledi ili kuifanya Wizara ya Nishati iwe kitovu cha ufanisi.

Mhandisi Mramba alitoa rai hiyo wakati akihutubia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Morogoro katika Ukumbi wa Ofisi za TAFORI.

Mramba alisema, Baraza la Wafanyakazi husaidia kuongeza tija na ufanisi wa taasisi pamoja na ushirikishwaji wa Wafanyakazi katika maamuzi ya pamoja mahala pa kazi.

Pia aliwajulisha wajumbe kuwa mwajiri anao wajibu wa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu ili kuendelea kuweka mazangira mazuri ya kazi kwa watumishi kwa kuongeza ari, ufanisi, wa kazi, kuongeza tija na hatimaye kuwezesha kufikia malengo yanayotarajiwa na taasisi.

Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba alisema, Watanzania wana matumaini makubwa katika kuona huduma katika Sekta ya Nishati zinaboreshwa ikiwemo upatikanaji wa umeme nchini kuwa wa uhakika muda wote.

Alisema, Serikali inatekeleza miradi 17 ya kimkakati kati ya hiyo 7 inasimamiwa na wizara ya nishati ikiwemo Bwawa la Kufua Umeme la Mwalimu Nyerere.

Amebainisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia Mradi Mkubwa wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ikifuatiwa na Bwawa la kuzalisha Umeme la Kidato lililopo mkoani Morogoro.

Aidha, aliwaasa wafanyakazi kutambua wajibu wao katika kazi badala ya kutanguliza masilahi binafsi kwa kuwa kila mmoja akitimiza wajibu wake. ufanisi wenye tija utapatikana na kupelekea malengo yaliyowekwa na Serikali katika utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati kufikiwa kwa wakati.

Watu 22 Mbaroni tuhuma za mauaji
Profesa Makubi ahimiza mikakati Bora hospitali ya rufaa Mwl Nyerere