Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watu 22 wanaotuhumiwa kushiriki kwenye mauaji ya watu mbalimbali wakiwamo wanaotuhumiwa kumuua Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Mahabusu ya watoto kwa kumnyonga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, alisema watu hao walikamatwa kufuatia msako maalumu uliofanywa na makachero wa jeshi hilo.

Amesema Jeshi hilo liliamua kufanya operesheni hiyo baada ya kuongezeka kwa wimbi la mauaji ya watu ndani ya mkoa huo yakiwamo yanayohusiana na visasi na wivu wa mapenzi.

Amesema katika tukio la mauaji ya Ofisa Maendeleo ya Jamii, Gloria Kibira (38) ambaye alikutwa amenyongwa ndani ya nyumba aliyokuwa anaishi ndani ya mahabusu ya watoto iliyoko Block T jijini Mbeya, watu wanne wanashikiliwa.

Dully Sykes afunguka alivyowanyanyua wasanii Bongo
Wizara ya Nishati kuwa kitovu Cha ufanisi