Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis Hamis,mwenye miaka 25,mkazi wa kijiji cha Ruponda wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi, inayowakabili maafisa saba wa jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara imeahirishwa hadi februari 22 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa tena.

Kesi hiyo iliyo chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mtwara,Lugano Kasebele,ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza januari 25 mwaka huu.

watuhumiwa hao ambao ni mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Mtwara mrakibu wa jeshi la polisi Gilbert Kalanje,mkuu wa kituo cha polisi mrakibu msaidizi wa polisi Charles Onyango,mkuu wa kikosi cha intelijensia mkoa wa Mtwara Mrakibu msiadizi wa polisi Nicholaus Kisinza,mganga Mkuu wa zahanati ya polisi mkaguzi wa polisi John Msuya.

Wengine ni mkaguzi msaidizi wa polisi Marco Mbuta,mkaguzi wa polisi Shiraz Mkupa pamoja na koplo Salimu Mbalu.

Katika mahakama hiyo hakimu mkazi mfawidhi Lugano Kasebele ameahirisha kesi hiyo ambapo itatajwa tena February 22 mwaka huu.

Mfanyabiashara huyo wa madini anatuhumiwa kuuawa mara baada ya kudai fedha zake zaidi ya shilingi milioni 33 zinazodaiwa kuchukuliwa na maofisa hao wakati wanamfanyia upekuzi.

Young Africans yalalamikia waamuzi Ligi Kuu
Dully Sykes afunguka alivyowanyanyua wasanii Bongo