Baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulioihusisha kampuni ya GSM na Shiriskiho la soka nchini TFF, Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ametoa kauli nzito.

GSM na TFF zilisaini mkataba wa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Novemba 2021, lakini Simba SC iligomea kutii masharti ya udhamini huo kwa kigezo cha kutaka ufafanuzi.

Ahmed Ally amesema kuvunjwa kwa mkataba wa pande hizo mbili, inatakiwa ichukuliwe kama somo la kufungua ukurasa mpya wa kuipa thamani Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inaongoza kwa ubora katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.

“Mwezi wa 1, 2 na 3 imepita hela haijawekwa na klabu hailalamiki bodi ya Ligi hailalamiki, Bodi ya Ligi iko pale kwa maslahi ya Vilabu, Bodi ilipaswa kumwambia TFF mbona huyo mtu haleti hela… ‘Basi Mimi nabandua logo kwenye jezi za vilabu vyangu na mabango siweki uwanjani mapaka hela iingie’ hilo halijafanyika tunakuja kusikia jana baada ya Mguto kusema,”


“Tuwatoe Yanga wanaonufaika moja kwa moja na huo mkataba hivi vilabau 14 vilishindwa kujipanga vikamwambia mwenyekiti wa bodi ya Ligi kuwa hatuweki mabango hatuvai wadhamini mapaka hela iingie,”

“Milioni tatu haitoshi hata maandalizi ya mchezo mmoja, achilia mbali mwezi mmoja na kama Prison huyo anayelia hana milioni tatu ni Timu ya Kushuka daraja, hatuwezi kuwa na Timu ambayo haiwezi kuwa hata na milioni tatu tutakuwa tunashindana nini sasa ?,”

“Katika sababu nane walizotoa za kuvunja mkataba ya nane ilikuwa ni Simba, inamaana hawa watu walitaka kuidhamini Simba, Tafsiri yake ni kwamba wamedhamini vilabu 15 wakiweka mabango 4 kwenye viwanja 15 ni sawa na mabango 60 inamaana hayo hayawatoshi mpaka wavunje mkataba kwa sababu ya Simba Sports”

Bernard Morrison aigomea Simba SC
Young Africans yalalamikia waamuzi Ligi Kuu