Rais wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya ‘UEFA’ Aleksander Ceferin, amepinga wazo Fainali za Kombe la Dunia kuchezwa kila baada ya miaka miwili na amependekeza kuwa na kikao cha wazi kwa viongozi watatu waasisi wa Super league.

UEFA hivi karibuni wameanzisha michuano mipya ya ligi ya timu za taifa ambapo mashindano hayo yanaenda sambamba na ligi za klabu ambazo zinachezwa kila baada ya miaka miwili.

Ceferin alinukuliwa akiwa kwenye mahojiano na Journal du dimanche akisema, “Nina uhakika Kombe la Dunia halitachezwa kila baada ya miaka miwili, kwa sababu ni wazo la kijinga.”

“Inaonekana kwangu kuwa shirikisho la mpira lingekuja na wazo la kupunguza kalenda ambayo wachezaji wanaangaika nayo.

“Tuna miezi mimgi ya kucheza kila majira ya joto, Kombe la Dunia, Kombe la Shirikisho na mashindano mengine mengi, miongoni mwa haya yataharibu mpira wa wanawake,” alisema Ceferin.

Biashara United yaivutia kasi Young Africans
Manara: Tunawakumbusha waamuzi wajibu wao