Kikosi cha Biashara United Mara, kimeweka kambi Magomeni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hatua ya dhidi ya Young Africans.

Biashara United Mara itakuwa ugenini dhidi ya Young Africans mchezo utakaopigwa Februari 15, Uwanja wa Benjamin Makapa jijini Dar es salaam.

Kocha Mkuu wa Biashara United, Vivier Bahati, amesema baada ya kumalizika mchezo wao dhidi ya KMC FC wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hawakutaka kurejea Musoma-Mara na badala yake wameendelea kubaki Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wa ASFC.

Amesema lengo kubwa la kubaki Dar es Salaam ni kufanya maandalizi kuelekea mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Young Africans ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kupata matokeo chanya na hatimaye kusonga mbele.

“Tuko jijini Dar es Salaam hatujaondoka, tumebaki kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Young Africans,” amesema Vivier. Amesema anayafanyia kazi madhaifu yaliyojitokeza katika michezo iliopita ikiwamo safu ya ushambuliaji kwa kuwa mchezo dhidi ya KMC FC walitengeneza nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.

Usimamizi matumizi ya mfumo wa anwani za makazi Mikononi mwa wakuu wa mikoa
UEFA yaiwekea ngumu FIFA