Mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani Cornell Iral Hynes Jr maarufu kwa jina la kisanii Nelly, ameomba radhi kufuatia kitendo cha kurusha kipande kidogo cha video kilichohusisha maudhui yasiyofaa, yanayomuonesha mwanamke akifanya mapenzi kwa njia ya mdomo.

Video hiyo aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story), amesema kuwa ni ya zamani na haikukusudiwa kuwekwa kwenye ukurasa wake huo wenye jumla ya wafuasi zaidi ya milioni 3 na kwamba hajui ni nani aliyeiweka.

Sakata la rapa huyo lilianza kuvuma zaidi siku ya jumanne kwenye mtandao Twitter baada ya kundi kubwa la watu kuona kipande hicho cha video kisichofaa kwa hadhira ambacho muda mfupi baadae kilifutwa.

“Ninaomba msamaha wa dhati kwa mwanadada huyo na familia yake, jambo lilitokea si lenye kufaa. Hii ilikuwa video ya zamani ambayo ilikuwa ya faragha na haikukusudiwa kuwekwa hadharani.” Alisema Nelly alipozungumza na TMZ.

Baada ya tukio hilo wengi wamekuwa na maswali ya Je, video hiyo ilikuwaje ikaingia kwenye akaunti ya Instagram ya nyota huyo? Jambo ambalo halijapata majibu licha ya hisia za wengi zikielekea kwenye upande wa dhana ya kuwa pengine akaunti ya Nelly imedukuliwa.

Kwa mujibu wa TMZ inasemekana timu ya msanii huyo inachunguza suala hilo na ina wasiwasi zaidi kuhusu maudhui ya faragha za Nelly pia yanaweza kuishia mtandaoni ikiwa ni pamoja na taarifa za fedha, nyaraka za kibinafsi pamoja na nywila (Passwords) za akaunti zake.

Mtawa afungwa kwa wizi wa pesa zaidi ya Mil 90
ATCL yaagizwa kufanya mapitio ya nauli zinazotozwa