Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema serikali kupitia wizara yake itafanya marekebisho ya sera, sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia sekta ya habari Ili zisiwe kikwazo katika kutekeleza majukumu ya wanahabari.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Februari 10,2022 wakati wa kikao na wahariri wa vyombo vya habari, kilichofanyika jijini Dar Es Salaam.

Waziri Nape ameilekeza idara ya habari maelezo kuandaa kikao kitakachohusisha wadau wa habari na wanahabari wenyewe Ili kuunda kamati itakayoshirikiana na serikali kuchambua sera hiyo na kupeleka mawazo mbele ya Bunge.

Amesema kuwa wakati sera ikiwa katika utaratibu wa marekebisho mambo mengine yataendelea kama kawaida katika kumlinda mwanahabari

Serikali yaonya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa
Hospitali ya Jeshi Dodoma kupokea fedha za Bajeti ya Serikali 2022/2023