Jeshi la zima moto na uokoaji Tanzania limemteua mwanamuziki Peter Msechu kuwa balozi wa zima moto nchini.

Uteuzi huo umefanyika mapema leo Februari 13 2022, muda mfupi baada ya zoezi la matembezi maalum yaliyofanywa na jeshi hilo, wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya iitwayo “Moto unazuilika Piga 114”.

Punde baada ya uteuzi huo Msechu ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kueleza namna alivyopokea uteuzi huo na moja kwa moja kuanza utekelezaji wa majukumu hayo.

“Mungu ni mwema wakati wote Jumapili ya leo tarehe 13.02.2022 nimetawazwa rasmi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuwa balozi wao. Hii kwangu ni heshima kubwa na ya kipekee kuwa miongoni mwa watakaopaza sauti katika kuhakikisha taarifa sahihi zenye manufaaa zaidi kwa wananchi hasa za kujikinga na majanga haya ya moto zinafika kwa weledi mkubwa.

Ameendelea kuamdika, “lengo likiwa kuhakikisha usalama wa Wananchi wote na Mali zao. Nimepokea uteuzi huu kwa unyenyekevu Mkubwa na sasa Rasmi naomba niwatangazie kuwa MOTO UNAZUILIKA.” ameandika Msechu. 

Kufuatia uteuzi huo Peter Msechu amekabidhiwa medali ya nishani na mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salam Amos Makalla.

Mchengerwa, Dkt. Abbasi Kushiriki Kilele cha Sauti za Busara Zanzibar.
Madiwani wataka uwiano walimu wa kike na wakiume