Mtu mmoja ameuawa na kundi la watu kwa madai ya kuchoma kurasa za Quran katikati mwa nchi ya Pakistan, Khanewal, katika tukio la hivi karibuni la vurugu zinazohusiana na kukufuru ama kukashifu dini nchini humo.

Polisi wanasema zaidi ya watu 80 wamekamatwa kuhusiana na mauaji hayo siku ya Jumamosi katika wilaya ya Khanewal katika mkoa wa Punjab.

Ripoti zinasema kuwa mtu huyo alikuwa chini ya ulinzi wa polisi kabla ya umati wa watu kumteka na kumuua kwa kipigo na Mwili wake kukabidhiwa kwa familia yake na mazishi yaliyofanyika siku ya Jumapili.

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan amesema suala hilo “litashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria” na kuomba ripoti juu ya maafisa wa polisi wanaotuhumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kumwokoa mtu huyo.

Mkuu wa kituo cha polisi mjini Tulamba ambako tukio hilo lilitokea, Munawar Gujjar, aliliambia shirika la habari la AP kwamba muathiriwa huyo alikuwa na matatizo ya akili kwa miaka 15 iliyopita.

Djuma Shaban kuivaa Mtibwa Sugar
Bwalya, Chama, Kanoute, Morrison wana kazi maalum Simba SC