Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amedokeza kwamba, ana matumaini ya suala la mkataba mpya la Mohamed Salah litafikia suluhisho, huku akisema wachezaji wanaofikia umri wa miaka 30, wanakuwa kwenye kiwango chao bora zaidi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri aliwahi kudokeza kwamba anataka kubaki Liverpool ingawa kulikuwa na ripoti kwamba wawakilishi wake wanataka dili la mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki.

Wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Group wamekuwa wakisita kutoa mkataba mnono kwa wachezaji ambao wanafikia umri wa miaka 30.

“Mwaka mmoja au miwili iliyopita wachezaji watatu wa mwanzo wa Ballon d’Or, pamoja na Salah ambaye alikuwa mdogo zaidi, wote walikuwa wakubwa wenye umri wa miaka 34 au zaidi,” alisema Klopp akiwaambia waandishi wa habari kuelekea mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Burnley.

“Lewandowski ana miaka 33, halafu Messi na Ronaldo wana 34 na 37 na kama una bahati zaidi ya kucheza bila ya kupata majeraha, unaweza kucheza kwa muda mrefu zaidi.

“Naamini suala la Salah litafikiwa tu makubaliano.”

Waziri Mkuu azungumza na wadau wa hifadhi ya Ngorongoro
Sumu kuvu tishio usugu wa dawa kwa binadamu na mifugo