Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa wabunge 19 wa viti maaalum wa CHADEMA wapo bungeni kihalali.

Amesema hayo leo Februari 14, 2022 katika mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari bungeni jijini Dodoma.

Amesema kuna masharti ya mbunge kuwa ndani ya bunge, na moja wapo ni awe amedhaminiwa na chama, hivyo wabunge hao wangekuwa hawana chama wasingekuwa bungeni.

Amefafanua zaidi kwamba hatua zinazosubiriwa ni kukamilika kwa michakato inayohusu uanachama wao, na kwamba bunge likipewa taarifa rasmi kwamba wamefukuzwa, basi hawatokuwa wabunge.

“Wabunge hao wa CHADEMA walifukuzwa uanachama na chama chao, lakini walikata rufaa kupinga uamuzi huo, na maamuzi ya rufaa yao bado hayajatolewa,”. Amesema Spika Tulia.

Sambamba na hayo Dkt. Tulia amesema kuwa suala la matangazo ya bunge kuruka mbashara linazungumzika, na kwamba wataangalia kwanini liliondolewa na umuhimu wake kurejeshwa sasa.

Rais Samia afanya mazungumzo na mkurugenzi wa UNESCO
Waziri Mkuu azungumza na wadau wa hifadhi ya Ngorongoro