Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda (Mb) leo Februari 15, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Sarah Gibson ofisini kwake Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine wamezungumzia kuendelea,a ushirikiano katika kutekeleza Mpango wa chakula Shuleni.

Prof. Mkenda amesema Wizara yake ipo tayari kuimarisha ushirikiano na Shirika hilo la kimataifa kwa lengo kubwa la kuwezesha mazingira ya ujifunzaji katika shule .

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani, Sarah Gibson ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuzindua
Mwongozo wa Chakula shuleni na kwamba WFP ipo tayari kusaidia utekelezaji wake kupitia tafiti walizofanya katika nchini mbalimbali zenye mpango kama huo.

Aidha, Gibson ameendelea kuelezea kuwa watasaidia pia katika suala la kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa chakula kwa wanafunzi shuleni na ushiriki wa Jamii.

Nasreddine Nabi: Tutacheza kwa tahadhari kubwa
Serikali yatoa Bilioni 1.4 ujenzi wa Daraja la Tembela