Daktari wa viungo wa Young Africans, Youssef Ammar amesema Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burkina Fasso Yacouba Songne, anatarajia kurejea Dimbani baada ya siku 45 (Sawa na mwezi mmoja na nusu).

Yacouba amekua nje ya Uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu, baada ya kuumia Goti, na kuepelekea kufanyiwa matibabu ya kiwango cha hali ya juu nchini Tunisia.

Ammar amesema Mshambuliaji huyo tayari ameanza mazoezi mepesi na muda si mrefu atajiunga na wenzake kwa ajili ya kuingia kwenye Program ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

“Licha ya Yacouba kupata nafuu pamoja na kuanza program ya mazoezi ya kukimbia mbio fupi na ndefu, lakini bado anaendelea na matibabu chini ya uangalizi wangu.”

“Bado hajapona vizuri, hivyo yupo chini ya uangalizi kwa hofu ya kujitonesha ili asirejee tena katika majeraha hayo ya goti. Kutokana na maendeleo yake hivi sasa, upo uwezekano wa kurejea rasmi uwanjani baada ya mwezi mmoja na nusu,” amesema Ammar.

Yacouba Songne, alipatwa na majeraha ya Goti kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting mwezi Novemba 2021.

Kauli tata ya ubatizo yasababisha Padri ajiuzulu
Kocha Simba SC aweka imani kwa John Bocco