Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa K. Mbega amewasilisha Hati za Utambulisho
kwa Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind , Ikulu (Rashtrapati Bhavan), mjini New
Delhi leo tarehe 16 Februari 2022. Baada ya kuwasilisha Hati hizo, Balozi Anisa
Mbega alifanya mazungumzo na Mhe. Rais Kovind. Wakati
wa mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Balozi Anisa Mbega aliishurukuru
Serikali ya India kwa misaada mbambali wanayoipatia Tanzania hususan, mikopo ya
masharti nafuu katika sekta ya maji pamoja na misaada mbalimbali kama vile
madawa na vifaa tiba pamoja na nafasi za mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa
watanzania. Aidha, alimpa Mhe. Rais Kovind salamu za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suhuhu Hassan ambapo Mhe. Rais Kovind
alishukuru kwa salamu hizo. Vilevile,
Mhe. Balozi Anisa Mbega aliahidi kuwa Tanzania itaendelea kudumisha uhusiano
uliopo wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji,
utalii na pia kufungua milango ya ushirikiano katika maeneo mengine. Rais
Kovind alisifu uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na India na akasisitiza
kuwa India itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye nyanja mbalimbali. Aidha,
alimuhakikishia Balozi Anisa Mbega kuwa Serikali ya India ipo tayari kutoa
ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa wepesi na ufanisi kwa
maslahi ya wananchi wa pande zote. |
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa .K. Mbega akisalimiana na Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind alipowasili kwenye Ikulu ya Rashtrapati Bhavan jijini New Delhi kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. |
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa K. Mbega akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind , Ikulu (Rashtrapati Bhavan), jijini New Delhi |
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa K. Mbega akiwa katika mazungumzo na Rais wa India, Mhe. Ram Nath Kovind kwenye Ikulu ya Rashtrapati Bhavan jijini New Delhi baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. |