Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu, amesema kuwa chama hicho kimepanga mikakati wa kupeleka wabunge zaidi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Shaibu amesema hayo wakati akizungumza na Dar24 katika mahojiano maalumu ambapo ameeleza mikakati ya ACT Wazalendo katika kukuza Demokrasia ndani na nje ya chama hicho na mikakati ya kuelekea katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
”Siasa za kiafrika licha ya kwamba tunapigania Ujenzi wa Taasisi hauwezi kudogosha nafasi ya mtu, tulikuwa na Tanzania tulikuwa na CCM lakini tulikuwa na Mwl. Nyerere, Rais Mwinyi alipoingia alikuwa na mambo yake vivyo hivyo Mwinyi hakuwa Mkapa, Mkapa hakuwa kikwete na Kikwete hakuwa Magufuli, ujio wa Mama Samia katika siasa zetu kulimaanisha kufungua ukurasa mpya,” amesema.
”sisi wapinzani tulikuwa tunatizama kwa umakini sura ya utawala wa Mama Samia katika mahusiano na vyama vya siasa kwa upande mmoja na mahusiano yake na wadau wa demokrasia kwa upande mwingine tulifarijika siku anaapishwa na hotuba yake tuliiskiliza na kuichambua,” ameongeza Shaibu.
”Alisema bayana anataka kufungua ukurasa mpya kwahiyo ukiniuliza kwa tathimini tangu kauli hiyo itoke mpaka sasa je kuna matumaini nitakujibu kwamba kuna matumaini kwa sababu jambo muhimu kuliko yote ni kuzungumza na Mama ameonesha kuwa yuko tayari kuzungumza,” amesema Shaibu.
Shaibu ameeleza kuwa ACT Wazalendo imekutana na Rais samia mara mbili baada ya uchaguzi wa konde kuvurugwa, “sisi tukijua tumeshinda na matokeo tunayo uchaguzi wa marudio…, tukaweka bayana kwa umma kwamba kama mambo ya Konde hayarekebishwi sisi tutafakari juu ya nafasi yetu katika serikali ya umoja wa kitaifa, tukapata nafasi ya kuonana na Rais Samia tukazungumza na Rais akachukua hatua.”
Ado Shaibu amekiri kuwa, kuwa Rais Samia kuzungumza na vyama vya sisa vya upinzani kumewapa mwanga kwamba hata uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu 2025 hautakuwa vilevile ndiyo maana Chama Cha ACT wazalendo wamependekeza kutangulia na tume huru ya uchaguzi.
”Licha ya upinzani mkali tunaoupata tumesema wazi kuelekea 2025 tutangulie na tume huru ya uchaguzi wengine wanasema tuanza na katiba sisi tumesema tuanze na tume kwanza kwasababu hatutaki uchaguzi wa serikali za mitaa usimamiwe na TAMISEMI”
Hili linaupa moyo kwam