Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amekutana na Sekretarieti ya Usalama Barabarani kwa lengo la kujitambulisha kwa wajumbe wa sekretarieti hiyo pamoja na kufahamu utendaji kazi wao.
Akizungumza na Wajumbe wa Sekretarieti hiyo kwenye ukumbi wa Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Sagini, amewapongeza kwa kazi nzuri wanazozifanya kwa kuhakikisha usalama barabarani unaendelea kuimarika na kwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara kwa wananchi na kupunguza ajali zinazopelekea vifo, majeruhi na uharibifu wa miundombinu.
“Ninawapongeza kwa utekelezaji wa majukumu yenu ya kuhakikisha kuna kuwepo hali ya usalama barabarani hasa kwa kutoa elimu kwa Watanzania nakupelekea kudhibiti ajali nchini” alisema.
Aidha Naibu Waziri Sagini amewataka wajumbe wa Sekretarieti ya Usalama Barabarani kuharakisha utekelezaji wa maelekezo waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan ya ununuzi wa vitendea kazi kwa kuyapa kipaumbele katika mpango kazi wao.
“Niwahimize, maagizo mnayopewa na Viongozi wenu na yale ambayo tumegizwa na Mheshimiwa Rais tuhakikishe tunayafanyia kazi haraka”.
Hata hivyo, Naibu Waziri Sagini imeihakikishia Sekretarieti hiyo kuwa, Wizara itaendelea kutoa ushirikiano na kuendela kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo na zitakazojitokeza kwa lengo la kuhakikisha kuwa, suala la ajali za barabarani linaendelea kupungua