Mlinda Lango la Manchester United, David de Gea Quintana amesema huenda akamaliza muda uliosalia kwenye soka lake akiwa na klabu hiyo yenye Maskani yake Uwanja wa Old Trafford.

Kwa mujibu wa takwimu, De Gea anashika namba mbili kwa kuzuia michomo iliyoelekezwa langoni kwake, nyuma ya Mlinda Lango wa Chelsea Kepa Arrizabalaga kwenye michuano yote kwa Walinda Lango wa Ligi Kuu ya England.

“Ukweli ni kwamba nilizaliwa Madrid, lakini mwisho wa siku ni jiji tu,” aliiambia UEFA.

“Sasa najihisi kama ninatokea Manchester, najihisi kama yeyote anayetokea Manchester sehemu unapopendwa ulipokaribishwa kama nyumbani kwako.”

“Sijioni nikiondoka Manchester United, nipo hapa kwa miaka najua chochote kinaweza kutokea kwenye maisha lakini sioni nikiondoka.”

Tangu aliposajiliwa Manchester United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid, De Gea ameshakaa langoni mwa Mashetani hao Wekundu katika michezo 365.

Waziri Mkuu azungumza na wabunge wa Marekani
Mganga mkuu wa serikali atoa onyo kwa wamiliki binafsi wa hospitali