Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene ameitaka ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuanza kuwachunguza na kuzichukulia hatua baadhi ya kampuni ya simu za mkononi pamoja na watumishi wake wanaovujisha taarifa za miamala ya wateja wao kwa wahalifu wa mitandaoni.

Akizungumza Februari 23, katika mafunzo ya makosa ya mitandao kwa mawakili wa Serikali, Waziri Simbachane amesema anashangazwa kwa kuona baadhi ya wahalifu wakijua taarifa za mteja aliyefanya muamala wa simu.

Waziri Simbachawene amesema kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya watumishi wa kampuni za simu sio waaminifu kwa kutoa siri za wateja kwa wahalifu na kusababisha wizi katika akaunti zao za fedha za baadhi ya mitandao.

“Kwani inawezekanaje kwa mhalifu akajua kwamba mtu fulani amefanya muamala wa kuhamisha fedha kama sio makampuni ya simu yanatoa siri lakini je mhalifuu anajuaje kama fedha imeingia kwa mtu na kwanini haya makampuni msiyakamate na kundi linaloathirika na wizi huo ni akimama,” amesema Waziri Simbachawene.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema baada ya mafunzo hayo wana imani kuwa mawakili wa Serikali watafanya kazi kwa weledi katika kushughulikia makosa ya kimtandao na kuondoa malalamiko mengi ya wananchi.

Mwakitalu amesema changamoto zilizokuwa zinakwamisha uendeshaji wa kesi za kimtandao ni uelewa mdogo kwa baadhi ya mawakili wa serikali jambo ambalo limesabaisha malalamiko kuwa mengi kwa wasomi hao kutokana na vitendo hivyo kuonekana kuongezeka siku hadi siku.

“Tumekuja Morogoro ili kuwapa uelewa zaidi na mawakili wa serikali wamekuwa wachache na umuhimu wa mafunzo hayo imeilazimu ofisi yetu kusimamisha shughuli ili kuhakikisha mhalifu asione kama kuna njia ya kufanikisha uhalifu wake,” amesema Mwakitalu.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Makosa ya Kimtandao Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Monica Mbogo amesema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuhakikisha waendesha mashtaka wanakuwa na uwezo wa kukabiliana na makosa hayo hasa wakati huu ambao teknolojia imekuwa kwa kiasi kikubwa.

Monica amesema sheria ya makosa ya mtandao sio mpya lakini kutokana na sababu za kukua kwa teknolojia mambo mbalimbali yamebadilika ikiwemo uendeshaji wa kesi na ushahidi unao kusanywa na kuwasilishwa vielelezo mahakamani.

Urusi yaanza kuishambulia Ukraine
Mkude, Mwenda waanza mazoezi Simba SC