Wizara ya Mambo ya Nje, imesema kuwa hadi sasa hakuna Mtanzania aliyepata madhara yoyote, kufuatia hali inayoendelea nchini Ukraine na kuwataka waendelee kuwa watulivu, wakati serikali ikiendelea kufuatilia usalama wao kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Ukraine.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini wa Wizara hiyo, Emmanuel Buhohela katika taarifa yake aliyoitoa leo Ijumaa, amesema serikali pia imewashauri Watanzania walioko huko, kufuata maelekezo yote yanayotolewa na Ukraine, pamoja na kuendelea kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden, ambao unaiwakilisha Ukraine kwa jambo lolote la dharura.

Wachangia damu Vinara kutambulika kielektroniki
Mzozo wa Ukraine: Mapigano makali karibu na Kyiv baada ya uvamizi wa Urusi