Nainu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew, amesema Wizara imeweka rekodi katika ujenzi wa Mkongo Taifa, ambapo kwa mwaka mmoja pekee Wizara hiyo imefanikiwa kujenga kilometa 4442 za Mkongo wa Taifa.

Naibu Waziri Kundo ameyasema hayo alipotembelea Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Singida.

Amesema kutokana na vijana wengi kusomea kazi hiyo na wataalamu wengi wa ndani ya nchi wakafanikiwa kujenga kilometa 350 na kampuni ya ndani ya nchi pamoja na kilometa nyingine 400 ambazo pia zimejengwa na kampuni ya ndani.

“Hapo utaona katika miaka kumi na kitu za ujenzi wa kilometa 8,000 sisi tunaenda kujenga kilometa 4442 ndani ya mwaka mmoja wa fedha, haya ndio Mapinduzi makubwa ya Sekta ya Mawasiliano”ameongeza Mhandisi Kundo.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kyaratu amesema kitendo cha Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushirikiana na TANESCO kutasaidia kuokoa fedha kutokana na miundombinu hiyo hiyo ya Tanesco kutumika kwenye mawasiliano.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Kundo amembatana na Mbunge wa Singida Kaskazini Ramadhani Ighondo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Paskas Muragiri.

Haji Manara aishangaa Simba SC
Ismail Rage: Sina shaka na Simba SC