Kocha Mkuu wa Simba SC Franco Pablo Martin ametamba kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane.

Simba SC itakua ugenini mjini Berkane-Morocco kucheza mchezo huo huku ikiwa kileleni mwa msimamo wa ‘Kundi D’ baada ya kuifunga ASEC Mimosas ya Ivory Coast na kutoka sare na USGN ya Niger.

Kocha Pablo amezungumza na wanahabari leo Jumamosi (Februari 26), ambapo amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri na kina matumaini ya kuendelea kuishangaza Afrika.

“Kesho tunakwenda kupambana na kumuonyesha kila mmoja Afrika kwamba tuna timu nzuri, wachezaji na makocha wazuri.” amesema Kocha Pablo.

Wakati Simba SC ikijiandaa kucheza dhidi ya RS Berkane kesho Jumapili (Februari 27), mchezo mwingine wa kundi hilo utakua kati ya USGN itakayokua nyumbani Nieamy-Niger ikicheza dhidi ya ASEC Mimosas.

Simba SC inaongoza msimamo wa Kundi D ikifikisha alama 04, ikifuatiwa na ASEC Mimosas yenye alama 03 sawa na RS Berkane, huku USGN ikiburuza mkia kwa kuwa na alama moja.

Roman Abramovic ajiuzulu Chelsea FC
Tanzania, kongo kuandaa mkutano wa wafanyabiashara