Benki kadhaa za Urusi zitaondolewa kwenye mfumo wa malipo wa kimataifa wa SWIFT.

Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alisema hatua hiyo itahakikisha kwamba benki zitasitisha uhusiano wake na mfumo wa kimataifa wa kifedha na Urusi ili kutatiza uwezo wake wa kufanya kazi kimataifa.

Ujerumani, Umoja Ulaya, Marekani na Uingereza zimetangaza vikwazo hivyo vipya dhidi ya Urusi.

Awali Ujerumani ilipinga hatua hiyo ikisema inaweza pia kuudhuru uchumi wa dunia.

Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana leo Jumapili kwa mara ya nne ndani ya wiki moja.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pia watashiriki mkutano kwanjia ya video kujadili msaada zaidi kwa Ukraine na hatua za adhabu kuelekea Moscow.

Mlipuko waripotiwa kutokea katika bomba la gasi Ukraine
Roman Abramovic ajiuzulu Chelsea FC