Chama cha Rais Uhuru Kenyatta Jubilee kimeamua kuwa mfanyabiashara Richard Ngatia ndiye atakayekuwa mgombea wao wa ugavana katika Kaunti ya Nairobi katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa wajumbe wa chama hicho, katibu mkuu anayeondoka Raphael Tuju alitangaza kuwa Ngatia atakuwa mgombea wa mrengo wa Azimio la Umoja kwa wadhifa wa Gavana wa Nairobi.

“Kama chama tumeamua ni Richard Ngatia. Kiongozi wetu wa chama Rais Uhuru Kenyatta pia atakuwa akithibitisha atakapohudhuria mkutano wetu Jumamosi,” amesema Tuju

Mbunge huyo wa zamani wa Rarieda alitoa sababu za wao kuamua kuwa Ngatia ndiye atakayepeperusha bendera yao, wakiwa na imani ya kuteka kiti hicho.

Kwa mujibu wa Tuju, jiji kuu la Nairobi ni shina la Kenya na hivyo basi uongozi wake lazima uoane na sura ya taifa kwani kaunti hiyo ndicho kitovu cha shughuli za serikali na makao ya balozi na wageni mbalimbali wa kigeni.

“Nairobi ndio mji mkuu na tunataka kuwa na uongozi unaodhihirisha sura ya nchini. Vyama tanzu vya Azimio vitatusaidia na Naibu Gavana na viti vingine,”

Ameongeza kuwa chama hicho tayari kimeanza mashauriano ya kupata atakayekuwa naibu wa Ngatia.

Afariki kwa kusimamisha uume muda mrefu
Vita Ukraine: Urusi yashusha makombora mawili usiku, shuhuda asimulia