Mwanamuziki mashuhuri kutoka Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P amethibitisha kuwa bado anampenda mwanasoshalaiti Eudoxie Yao miezi kadhaa baada ya ripoti kuenea kuwa wametengana.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Grand P mwanasoshalaiti huyo aliandika ataishi kumpenda mwanadada huyo aliyebarikiwa na makalio makubwa kutoka Ivory Coast na kudhihirisha upendo wake kwake usio na mwisho.

“Wewe na mimi ni kwa maisha. Shukran” Grand P alimwandikia Yao.

Haya yanajiri takriban miezi miwili baada ya Grand P kudai kapokonywa kipenzi chake na mwanamuziki Roga Roga kutoka Congo baada ya Picha za Yao akijiburudisha na Roga Roga kuenezwa mitandaoni na kumtia Grand P hofu kuwa huenda  msanii huyo alikuwa amempokonya penzi lake.

Grand P ambaye ana maumbile ya kipekee alimpatia Roga Roga onyo kali dhidi ya kuendeleza mahusiano na mkewe.

“Ndugu yangu Roga Roga nakuheshimu sana wewe na watu wote wa Kongo… Lakini  njia unayotaka kufuata si ya kupendeza kwako, usifurahie kuwa karibu na mke wangu la sivyo nitachukua hatua mbaya. Hii ni onyo, Asante!” Grand P aliandika.

Takriban miezi sita iliyopita Yao alikuwa ametangaza kutengana kwake na Grand P ila baadae walionekana pamoja mara kwa mara, hakikisho kuwa walirudiana.

Hivi majuzi hata hivyo, Yao alimtaja bilionea huyo kama mpenzi waliyeachana baada ya kumuona akijiburudisha na wanadada wengine ndani ya bwawa la kuogelea.

Waziri Jafo atoa siku 14 tatizo hili lipatiwe ufumbuzi
Afariki kwa kusimamisha uume muda mrefu