Mwanamitindo wa Ukraine Anastasia Lenna amabye habari zake zimesambaa kwa kasi kubwa kote mitandaoni baada ya kupiga picha akiwa amevalia mavazi ya jeshi la Ukraine huku akiwa ameshikilia bunduki amepata wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao yake ya kijamii.

Lenna ambaye aliiwakilisha nchi yake kwenye shindano la urembo la Miss Grand International 2015 aliweka picha hiyo kwa ishara ya kuwa tayari kwa mapambano ya kuitetea nchi yake katika vita dhidi ya taifa la Urusi.

“Yeyote atakayevuka mpaka wa Ukraine kwa nia ya kuvamia atauawa!” alinukuu picha ya askari wenye silaha wakifunga barabara. Chapisho lililowekwa mtandaoni muda mfupi kabla ya Urusi kuivamia Ukraine wiki iliyopita, Februari 24.⁣

Wakati anaweka chapisho hilo kwa mara ya kwanza, mrembo Lenna alikuwa na jumla ya wafuasi 75,000 kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, lakini muda mfupi tu baadae, mwanamitindo huyo  alijipatia zaidi ya wafuasi 211,000, jambo lilitoa taswira ya kuwa ujumbe uliobebwa ndani ya picha ya mrembo huyo umewavutia wengi.

Ukraine ni jamhuri ya zamani ya Soviet inayopakana na Urusi na Umoja wa Ulaya, hii sio nchi mwanachama wa mataifa ya NATO, lakini ni nchi mshirika ambayo inaweza kuruhusiwa kujiunga na muungano huo wakati fulani katika siku zijazo.

Maombi na dua za mamilioni ya watu Duniani kote ni kushuhudia amani inarejea kati ya mataifa hayo ili kuepusha athari mbali mbali zitokanazo na machafuko.

Lwanga: Nipo tayari kuitetea Simba SC
Ahmed Ally: Msihofu wala msihuzunike