Kocha Mkuu wa Azam FC Abdihamid Moalin amesema hana njia ya mkato kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union utakaopigwa leo Jumanne (Machi Mosi), Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Azam FC wanashuka kwenye Dimba lao la Nyumbani mishale ya saa moja usiku, huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Biashara United Mara kwa mabao 2-0.

Kocha Abdihamid Moalin amesema mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union una umuhimu mkubwa sana kwao, na ana matarajio ya kuibuka na ushindi kutokana na maandalizi alioyafanya, baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Biashara United Mara.

“Mchezo na Coastal tumejipanga kushinda, itakuwa ni mechi ngumu lakini hatuna budi kupambana, ili kutimimiza lengo la kupata alama tatu.”

“Tumepoteza mchezo uliopita kwa makosa madogo yaliojitokeza, nimejitahidi kuyarekebisha na nina imani kubwa leo tutapambana vilivyo na kufanikisha furaha kwa mashabiki wetu.” amesema Kocha Abdihamid Moalin

Coastal Union nao watakua na mtihani wa kurekebisha makosa yao, baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold FC.

Simba SC Vs Biashara United kupigwa Ijumaa
Lwanga: Nipo tayari kuitetea Simba SC