Bodi ya Ligi Tanzania Bara ‘TPLB’ imesogeza mbele mchezo wa Mzunguuko wa 16 kati ya Mabingwa watetezi Simba SC dhidi ya Biashara United Mara uliokua umepangwa kuchezwa keshokutwa Alhamisi (Machi 03).

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally zimeeleza kuwa, mchezo huo sasa utapigwa Ijumaa (Machi 04), Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Mabadiliko hayo yamefanywa ili kutoa nafasi kwa Simba SC kujiandaa na mchezo huo, baada ya kuwasili leo Jumanne (Machi Mosi), ikitokea nchini Morocco ikipitia Dubai.

Jumapili (Februari 27) Simba SC, ilicheza mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco na kupoteza kwa mabao 2-0.

Simba SC inayotetea Ubingwa wa Tanzania Bara, itacheza dhidi ya Biashara United Mara, huku ikikumbuka sare ya bila kufungana iliyopatikana kwenye mchezo wa Duru la Kwanza uliozikutanisha timu hizo mjini Musoma mkoani Mara.

Serikali yakubali mipango ya TFF
Kocha Azam FC aivizia Coastal Union