Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa Amesema Serikali haijalipia kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika Jiji la Dubai.

Amesema tangazo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kaifanya Dubai na umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu

Jay-Z aongoza wana Hip-Hop waliovuta mkwanja mrefu 2021
Keiv inatafakari 'kuishambulia' Belarusi