Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepiga marufuku Warusi kuhamisha fedha nje ya nchi, wakati akijaribu kuzuia kushuka kwa thamani ya fedha hizo, kufuatia kuwekwa kwa vikwazo.

Katika taarifa yake kupitia tovuti ya Kremlin, Putin amesema uhamisho wa fedha bila kufungua akaunti ya benki kwa kutumia njia za elektroniki za malipo zinazotolewa na wauzaji wa kigeni wa huduma za malipo pia zitapigwa marufuku.

Zaidi ya hayo, wakazi wa Urusi wamepigwa marufuku kutoa mikopo ya fedha za kigeni kuanzia Machi mosi kwa wakazi na kwa wasio wakazi.

Meli iliyobeba magari ya kifahari 4,000 yazama
Jay-Z aongoza wana Hip-Hop waliovuta mkwanja mrefu 2021