Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameunga mkono hadharani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kainerugaba, ambaye ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu ya Uganda, ndiye afisa mkuu wa kwanza wa kijeshi kutoka barani Afrika kuunga mkono hatua ya Rais Vladmir Putin kurusha makombora Ukraine kupitia ujumbe aliochapisha kwenye kitandazi chake rasmi cha Twitter, siku ya Jumatatu, Februari 28.

Kainerugaba alisema, “Binadamu wengi (ambao si wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine. Putin yuko sahihi kabisa!” aliandika.

Cha Maana Sasa Sio Mali, Milki, Majumba au Biashara zako Bali Maisha Yako Kamanda huyo alielezea sababu ya msimamo wake akisema, “Wakati USSR ilipoweka makombora yenye silaha za nyuklia nchini Cuba mwaka 1962, nchi za Magharibi zilikuwa tayari kulipua ulimwengu juu yake. Sasa Nato ikifanya hivyo wanatarajia Urusi kufanya tofauti.”

Hata hivyo Ujumbe wake ulizua hisia mseto kwenye mtandao wa kijamii huku Waganda wengi wakimuunga mkono na wengine wakimkosoa na kumkumbusha kuwa Waafrika wanaoishi Ukraine pia wameathiriwa na vita hivyo.

Umoja wa kanda ya Afrika Magharibi (ECOWAS) umelaani uvamizi wa Urusi, huku Umoja wa Afrika(AU) ukighadhabishwa na taarifa za ubaguzi kwa raia wa Kiafrika nchini Ukraine baada ya taarifa kuibuka kuwa Waafrika wanaoikimbia Ukraine, hawapewi huduma kama wengine na hata wakati mwingine wanazuiawa kuondoka.

GGM yapongezwa na Bunge kwa kusimamia masuala ya UKIMWI
Taharuki ya ugaidi yasitisha shughuli za mahakama Nchini Kenya